MHUDUMU na mke wa mwenye nyumba ya kulala wageni Silent Inn iliyoko
mjini Mugumu wilayani Serengeti amenaswa na pembe nne za meno ya tembo
akiwa amechimbia porini .
Tukio hilo ambalo ni mwendelezo wa ukamataji wa nyara za taifa
limetokea januari 17,majira ya saa 4:00 usiku katika eneo la Chamoto
Mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu mwaka huu limethibitishwa na kamanda wa
polisi mkoa wa Mara.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alimtaja mtuhumiwa
huyo kuwa ni Rebeca Julius (32)mkazi wa eneo la Chamoto mjini Mugumu.
Alisema kukamatwa kwake kunatokana na mtego uliowekwa na askari polisi
na Tanapa wakijifanya wanunuzi wa men ohayo ambayo amedai ni makubwa
ili thamani yake haijajulikana.
“Wakiwa doria ya pamoja huku wameweka mtego huo waliweza kumnasa
kirahisi mgtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amechimbia meno hayo
porini”alisema kamanda.
Inasemekana kuwa wakati analeta men ohayo alikuwa na watu wawili
waliomsaidia kuchimba ambao walifanikiwa kutoroka baada ya kubaini
kuwa mteja wao alikuwa ni askari.
Mwananchi Jumamosi imebaini kuwa mtuhumiwa huyo novemba 11,2010
alikamatwa na magunia 2 ya nyama kavu yenye jumla ya vipande 50 akiwa
anapeleka wilayani Tarime.
Katika tukio hilo akiwa ndani ya gari la abiria lenye namba za usajiri
T 185 ASJ Hiace katika kijiji cha Nyansurura alikamatwa na kufunguliwa
jalada MUG/IR/2901/2010 kisha kufikishwa mahakama ya wilaya kesi namba
ECO,NO 66/2010 ambayo haijajulikana ilivyokwisha.
Pia katika tukio lingine mwaka 2011 katika nyumba hiyo ya kulala
wageni ya Silent Inn walikamatwa na meno mawili ya tembo wakiwa
wameyafukia chini na kufikishwa polisi na mahakamani lakini aliachiwa
tena.
Habari za uhakika zinadai kuwa katika tukio lingine mtuhumiwa huyo
ambaye anahusishwa na mtandao wa wawindaji wa tembo kutoka Kigoma na
maeneo mengine aliwahi kupokea watuhumiwa wengine waliokamatiwa hotel
ya Galaxy Motel na Leopard wakiwa na meno ya tembo na mzani wa
kupimia.
Kushamiri kwa biashara hiyo kunatokana na watuhumiwa kukamatwa kisha
kuachiwa katika mazingira tata na kuendelea na biashara hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment