Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, aliviambia vyombo vya
habari kuwa, tayari wameshaanza msako huo katika operesheni maalum
iliyoanza hivi karibuni. Amesema mbali na makahaba hao pia wamekusudia vilevile kuwakamata wamiliki wa nyumba zinazojihusisha na biashara hizo. Amesema wamiliki wa nyumba hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria kujihusisha na biashara hizo hata kama akibainika kumpangisha mpangaji yeyote anayejihusisha na kuuza mwili wake. Amesema jeshi hilo limejipanga vilivyo kukabiliana na biashara hiyo ambayo inasababisha ongezeko la maambuzi mapya ya virusi vya Ukimwi. Amesema katika operesheni hiyo tayari wameshaweza kuwakamata makahaba zaidi ya 35 waliokamatwa maeneo tofauti ya Kinondoni. |
||
|
||
|
Monday, January 14, 2013
MAKAHABA 35 WAKAMATWA KINONDONI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment