Watu hao wanashikiliwa kutokana na tukio la mauaji lililotokea siku ya
Jumatano tarehe 09/01/2013 majira ya saa 04:00 mchana katika kitongoji
cha Mtakuja kata ya Chitemo katika Wilaya ya Mpwapwa.
Katika tukio hilo walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la NELSON S/O NYAGULU mwenye umri wa miaka 32, mkulima wa Chitemo
kwa kupigwa na risasi ya Bunduki aina ya Gobore tumboni na mtu
aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KALANI.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba tarehe 08/01/2013 huko katika
kijiji cha Chitemo kulikuwa na mnada, ambapo mvua ilinyesha sehemu moja
ya kitongoji cha Mtakuja, sehemu ambayo alikuwa anaishi mzee mmoja
aliyejulikana kwa jina la LEONARD S/O NYAGALU, Miaka 70, Mgogo.
Kwa vile mvua hiyo haikunyesha sehemu kubwa katika kitongoji hicho
inasemekana Mwenyekiti wa Kijiji JAVAN S/O MZAZI, Miaka 40, Mgogo,
aliibua hoja kuwa kwa nini mvua inyeshe eneo moja tu analokaa Mzee huyo
na kuacha kunyesha sehemu nyingine katika eneo hilo na kuwahamasisha
wenzake kwenda kwa Mzee Nyagalu akawaeleze vizuri.
Majira ya 23.00 hrs usiku wakakusanyana na kuelekea kwa Mzee Nyagalu,
Walipofika Mzee huyo alisikia watu wakizungumza nyumbani kwake hivyo
akavunja ukuta na akatoroka.
Inadaiwa kuwa kundi hilo lililokuwa limeongozana na Mwenyekiti wa Kijiji
hicho waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mke wa Mzee Leonard Nyagalu
na kuanza kumpiga ili aonyeshe aliko mume wake, waliposhindwa kumpata
wakabomoa nyumba na kuichoma moto.
Wakati wanafanya tukio hilo, walijitokeza watoto wa Mzee Leonard S/O
Nyagalo, mmoja wao akiwa ni NELSON S/O NYAGALU, Miaka 32, Mgogo na ndipo
nao wakaanza kupigwa.
Kwa mujibu wa watu walikuwa katika tukio hilo walisema ilisikika sauti
ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KARANI akisema sasa
mmetangaza vita na akafyatua gobore na risasi zikampata NELSON S/O
NYAGALU tumboni zilizopelekea kupoteza maisha wakati anapata matibabu.
Baada ya kufyatua risasi toka katika gobole Bw. RASHID S/O KARANI
aliwaaga wenzake kuwa anakwenda kujisalimisha Polisi lakini hadi sasa
hajaonekana na jitihada za kumtafuta pamoja na silaha aliyotumia
zinaendelea.
Majina ya wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika tukio hilo ni kama ifuatavyo:-
1. Dickson S/O Chimosa, Miaka 52, Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Chitemo.
2. Javan S/O Mzazi, Miaka 44, Mgogo, Mwenyekiti wa Chitemo.
3. Robert S/O Lusije, Miaka 51, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
4. Donald S/O Mponi, Miaka 33, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
5. Daniel S/O Mwamba, Miaka 24, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
6. Maneno S/O Ngaile, Miaka 36, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
7. Thomaso S/O Nyagalo, Miaka 28, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
8. Gilbert S/O Lugaje, Miaka 39, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
9. Aden S/O Simon, Miaka 33, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
10. Malolo S/O Sanja, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
11. Sospeter S/O Sanja, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
12. Jocktan S/O Chilomo, Miaka 40, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
13. Keneth S/O Ngaile, Miaka 38, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
Aidha siku ya Jumamosi tarehe 05/01/2013 majira ya 08:00 asubuhi
kulikuwa na tukio la mauji lililotokea katika Kitongoji cha Magungu,
Kijiji cha Mpendo, Kata ya Mpendo Tarafa ya Kwa Mtoro Wilaya ya Chemba
Mkoa wa Dodoma.
Ambapo mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la TONY S/O SOKOINE mwenye
umri wa miaka miwili na nusu (2.5), mkazi wa Kijiji cha Mpendo alifariki
dunia baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa na kisu shingoni kilichorushwa
na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa jina la SOMEI S/O REMENDA mwenye
umri wa miaka mine (4) mkazi wa Kijiji cha Mpendo.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha Kifo hicho ni kwamba
marehemu na mtuhumiwa walikuwa wanacheza nje nyumbani kwao kwa akina
SOKOINE S/O RENENDA ambapo mtuhumiwa alirusha kisu kwa lengo la kumuua
ndege aliyekuwa juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yao, ndipo kisu
huchi kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi
marehemu kwa kumchoma shingoni na kusababisha kifo chake.
DAVID A. MISIME - ACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
No comments:
Post a Comment