LA LIGA jana ilimshuhudia Supastaa Lionel Messi
akiifungia Timu yake Barcelona Bao mbili na kuipa ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya
Real Betis huku yeye akivunja Rekodi ya tangu Mwaka 1972 ya Straika wa Germany
Gerd Muller ya kufunga Bao 85 ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda kwa yeye
kufikisha Mabao 86 na wakati huo huo Straika hatari wa Atletico Madrid Radamel
Falcao akipiga Mabao 5 katika Mechi moja walipoifunga Deportivo La Coruna Mabao
6-0.
+++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA:
-Lionel Messi=Bao 23
-Radamel Falcao=16
-Ronaldo=13
-Aduriz=9
+++++++++++++++
Matokeo hayo ya jana yameifanya Barca izidi kupaa
kileleni ikiwa na Pointi 43, Atletico Madrid
nafasi ya Pili Pointi 37 na Real Madrid ni wa Tatu Pointi 32.
MSIMAMO-Timu za Juu
[Kila Timu imecheza Mechi 15]
1 Barcelona
Pointi 43
2 Atletico Madrid
37
3 Real Madrid
32
4 Malaga
25
5 Real Betis 25
6 Levante 24
7 Getafe
23Bottom of Form
No comments:
Post a Comment