MAREHEMU JOSEPH MWASOKWA
MNAMO TAREHE 09/12/2012 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO
MAENEO YA BLOCK - T JIJI NA MKOA WA MBEYA. JOSEPH S/O NELSON MWASOKWA, MIAKA
78,KYUSA, AFISA USALAMA WA TAIFA MKOA WA MBEYA [MSTAAFU] NA MKAZI WA BLOCK T .
ALIGUNDULIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE KWA KUKATWA NA KITU CHENYE MAKALI
KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU
ULIKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA SEHEMU ZA SHINGONI, KICHWANI MABEGANI NA MKONO WA
KUSHOTO. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA KITU CHOCHOTE CHA MAREHEMU KILICHOCHUKULIWA
KWANI MAREHEMU ALIKUTWA NA PESA TASLIMU TSHS 107,000/= DOLA 200 ZA KIMAREKANI NA
SIMU MOJA YA MKONONI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA WAKATI AKIINGIA KWENYE GETI
LA NYUMBA YAKE. KWA MARA YA MWISHO MAREHEMU ALIRUDI NYUMBANI NA JIRANI YAKE
MAJIRA YA SAA 20:00HRS TOKA SOWETO KUTAZAMA FAINALI YA MPIRA WA MIGUU KOMBE LA
CHALLENGE KATI YA UGANDA NA KENYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE
KATIKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA
|
R.I.P NELSON MWASOKWA
ReplyDelete