Monday, December 17, 2012

JUBILEE YA MIAKA 50 YA SHULE YA MBEYA DAY YAFANA MBEYA NA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 58 ZACHANGWA

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akiwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigalla  katika maandamano ya Jubilee ya miaka 50 ya shule ya sekondari Mbeya Day

Wanafunzi wa shule ya mbeya sekondari wakipiga ngoma kuongoza maandamano hayo ya jubilee ya kutimiza miaka 50 ya shule hiyo
Mgeni rasmi katika jubilee hiyo Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akivikwa skafu na mwanafunzi kuashiria kukaribishwa shuleni hapo
Mgeni rasmi na mheshimiwa mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi wakitembelea shule hiyo ya Mbeya day ilikujionea maendeleo ya shule hiyo kwani mgeni rasmi na mweshimiwa mbunge walisoma hapo darasa moja
Hapo mgeni rasmi akionyeshwa jinsi ya majengo ya shule hiyo yalivyo sasa
Mgeni rasmi katika jubilee hiyo Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akipanda mti kama kumbukumbu ya kufika shuleni hapo
Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla akipanda miti
Baadhi ya wanafunzi waliosoma zamani katika shule hiyo wakiwa pamoja katika sherehe ya kutimiza miaka 50 ya shule ya sekondari Mbeya Day
Wote hawa niwanafunzi waliosoma shule ya Mbeya sekondari
Baadhi ya watumishi wa shirika la nyumba waliungana na murugenzi wao katika kuadhimisha miaka 50 ya shule hiyo
Wazazi pamoja na waandishi wa habari mkoa wa mbeya walihudhuria sherehe hiyo
Wanafunzi wa shule ya Mbeya sekondari
Ilikuwa ni furaha ya aina yake kukutana wanafunzi karibia wote waliosoma shule hiyo hapa wakipongezana 
Wanafunzi wakiimba wimbo wa taifa
Hapa kwaya ya shule ikiimba wimbo maalumu wa kutimiza miaka 50 ya shule hiyo
Mgeni rasmi katika jubilee hiyo Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu ametoa kiasi cha shilingi milioni 20 kuchangia ujenzi wa maabara ya kisasa shuleni hapo ili maabara hiyo ikamilike kinahitajika kiasi cha zaidi ya shilingimilioni 150
Mkuu wa wilaya Mbeya ametoa kiasi cha shilingi milioni 2 kuchangia ujenzi huo wa maabara ya kisasa
Mheshimiwa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ameta kiasi cha shilingi milioni 1 na vifaa vya michezo
Mkurugenzi wa kampuni ya Celsoutions Sammy Zanny ambaye pia ni mwanafunzi aliyesoma hapo ametoa zaidi ya shilingi milioni 3 tatu kashi kuchangia ujenzi wa mahabara hiyo ya kisasa shuleni hapo
Mkurugenzi wa kampuni ya Celsoutions Sammy Zanny akimkabidi mgeni rasmi pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 3
Mgeni rasmi katika jubilee hiyo Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akiwashukuru wote waliochangia na kufikisha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 58 zilizopatikana leo
Mwandishi wetu Joseph Mwaisango inaelekea akimsisitizia kitu mgeni rasmi mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo

No comments:

Post a Comment