Waziri wa nchi ofisi ya Rais
mahusiano na Uratibu Mh.Steven Wassira aligawa hati 97za ardhi za kimila kwa
wananchi wa wilaya ya ludewa katika kijiji cha Amani kupitia mpango wa
MKURABITA.
Akitoa hati hizo Wassira
aliwaasa wananchi hao kuwa ardhi ni mali hivyo kila mwananchi wa
kawaita anapaswa kuwa na hati hizo ili kuweza kukopesheka na taasisi za
kifedha.
Bw.Wassira alisema umiriki wa
ardhi nchini ni wa kila mmoja ila kinachotakiwa ni kuiendeleza ardhi hiyo na
kuwa makini na wawekezaji wadanganyifu.
Alisema vijana wanapaswa
kuunda vikundi ili waweze kukopesheka na kuzalisha mazao yatakoyoweza uzika
katika migodi iliyoko jirani na kijiji hicho.
Katika hatua nyingine
Bw.Wassira aliweza kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji cha
shaurimoyo kata ya Lugarawa ambayo imejengwa na mradi wa TASAF.
Pia alifungua vyumba vinne
vya madarasa ikiwa na nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Songambele
iliyoko Ludewa kijijini kwa ufadhiri wa TASAF.
Aidha Bw.Wassira
alisikitishwa na tabia ya watu wanaoharibu mazingira kwa kuchoma moto ovyo
misitu katika kijiji hicho.
Alisema upataji wa hati hizo
kupitia MKURABITA unatakiwa uendane na utunzaji wa mazingira na si vinginevyo
ili kuepusha hali ya ukame.
Hata hivyo aliwaasa wananchi
hao kuzitunza hati hizo za kimira kwani ni ukombozi kwa vizazi vyao ambapo
hawataweza ingiliwa na mtu yeyote katika maeneo yao.
kwa hisani ya habari Ludewa
No comments:
Post a Comment