Saturday, October 27, 2012

SERIKALI YAONGEZA VOCHA ZA RUZUKU


Ni katika kupunguza adha kwa wakulima
Halmashauri zote nchini zapewa
MKUU wilaya ya Njombe naye asema wilaya yake imenufaika pia.
 Serikali Imeongeza Vocha za Ruzuku Kwa Wakulima Kupitia Mawakala Wake Ili Kukabiliana na Upungufu Uliojitokeza Baada ya  Vocha Zilizotolewa Awali  Kwa Wakulima  Kuonekana Hazikidhi Mahitaji ya Wakulima Hapa Nchini.
Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo za Kilimo Wilaya ya Njombe Ambaye Pia ni Mkuu wa Wilaya Bi.Sara Dumba Amesema Katika Ongezeko Hilo Wilaya ya Njombe Imepata Ongezeko la Vocha Elfu Kumi na Moja Mia Tano Ambazo Zitagawanywa Katika Halmashauri Zote za Wilaya Hiyo.
Amesema Licha ya Kuwa Zoezi la Usambazaji Vocha Hizo Kwa Wakulima Limeanza Tangu Mwezi  Agosti Mwaka Huu, Serikali Imeona ni Vema Kuongeza Kiwango Hicho Kwa Ajili ya Kukabiliana na Tatizo la Upungufu wa Mbolea Wakati Zoezi Hilo la Usambazaji Likiendelea.

Aidha Bi. Dumba Ameeleza Kuwa Vocha Hizo Zitawanufaisha Zaidi Makundi Maalumu Wakiwemo Wazee , Watoto Yatima Pamoja na Watu Ambao Hawana Uwezo wa Kumudu Gharama za Kununua Mfuko Mmoja.
Katika Hatua Nyingine Mwenyekiti Huyo wa Kamati ya Penbejeo Wilaya Amewashauri Watu Wenye Uwezo Wanunue Pembejeo za Kilimo Kwenye Maduka Yanayouza Pembejeo Hizo.

No comments:

Post a Comment