Wananchi wa kijiji cha Kiyogo wilayani Ludewa Katika mkoa wa
Njombe wameilalamikia Serikali ya wilaya hiyo kwa kuwasahau kwa muda mrefu hali
inayowafanya waishi kama wako kisiwani kutokana na kukosa huduma za msingi
ikiwemo maji safi na salama.
Kijiji hicho ambacho tokea enzi za mababu hakijawafi pata
maji safi na salama ya bomba wananchi wake wamekuwa wakiugua magonjwa ya
matumbo kutokana na kutumia maji yam to Ruhuhu ambayo ni machafu yanayotumika
na wachimba madini kuoshea madini maeneo ya wialaya ya Mbinga na kijiji cha
Amani.
Akizugumza mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Thomas Magnas
alisema anashindwa kuamini kama Serikali haiwatambui wananchi hao kwani kijiji
hicho kimesajiriwa kisheria na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
lakini wanaishi kama wakimbizi.
Bw.Magnas aliyema ni miaka mingi sasa wananchi wa kijiji
hicho wanakunywa maji machafu kuanzia rangi ya maji hayo inatisha kutokana na
chanzo cha mto huo kuwepo wachimba madini wanaoyachafua maji hayo hali hiyo
imesababisha watu wengi wa kijiji hicho kupoteza maisha kutokana na homa za
matumbo.
“Tunaishi kama si Watanzania kutokana na kutokuwa na
majisafi na salama kwani hata dhahanati wananchi tumejitolea kuijenga lakini
hakuna wafanyakazi hivyo inatupasa kutembea kilimita 15 kufuata huduma hiyi
pindi tunapougua”,alisema Bw.Magnas.
Alisema kutokana na magonjwa ya mripuko yanayosababishwa na
uchafuzi wa maji hayo huwa inawalazimu kwenda vijiji vya jirani ambavyo ni
Lihagule na Masasi wakati mwingine hulazimika kuvuka mto Ruhuhu kwa mitumbwi na
kwenda mkoa jirani wa Ruvuma kufuata huduma za Afya.
Katika huduma za Afya wananchi hao waliilalamikia Serikali
kwa kutowatendea haki hasa akinamama wajawazito kutokana na umbali wa vituo vya
Afya kani baadhi ya akina mama hujifungulia njiani hali hiyo huwafanya wahudumu
wa Afya kuwatoza kiasi cha shilingi elfu tano kwa yeyote aliyejifungulia njiani
bila kujali umbali wa kijiji hicho mpaka katika vituo hivyo.
Akizungumza kwa uchungu Bi.Gaudesia Jonh alisema wamekuwa
wakinyanyaswa kupata huduma za Afya wanapokwenda katika zahanati za vijiji vya
jirani hasa nyakati za usiku kwa kuulizwa wanatoka kijiji gani hali hiyo
inawakosesha amani kwani wakati wa chaguzi mbalimbali za viongozi huahidiwa
huduma za jamii lakini wakishachagua hakuna kinachoendelea.
Bi.Gaudesia alisema hali hiyo ya kutozwa shilingi elfu tano
katika vituo vya Afya kwa kosa la kijifungulia njiani si kosa la akina mama hao
bali ni kosa la Serikali yao kwani wamejenga zahanati nzuri lakini haina
wafanyakazi hali ambayo inawalazimu kutembea kilometa 15 kufuata huduma za Afya
ya mama na mototo.
Wananchi hao wlisema bado wanamaswali mengi vichwani mwao
kama kweli Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961 na kusherekea miaka 50 ya uhuru
huo wakati kunawananchi ambao hawana huduma muhumu kama zahanati,maji safi na
salama na ujenzi wa shule ya msingi isiyo na sakafu yenye saruji.
Walisema kijiji hicho kinashule ya msingi ambayo ilijengwa
na wananchi miaka mingi iliyo pita na kusaidiwa na shirika la Consein kwa
kupewa mabati lakini tokea hapo Serikali haikuitupia jicho shule hiyo zaidi ya
kuwaleta walimu watatu na wakati mwingine hubaki walimu wawili.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiyogo bado wanasiriba kwa tope
sakafu ya shule yao hali ambayo inawakatisha tama ya kusoma kwani vijiji vya
jirani kuna shule nzuri zenye walimu wakutosha lakini kwa kijiji chao hali hiyo
imekuwa kitendawili.
Bw.Magnas alisema mpaka sasa wamejenga madarasa manne na
ofisi mbili za walimu kwa lengo la kuihamisha shule ya awali kutokana na shule
hiyo kuwa na nyufa kubwa ambazo
zinahatarisha usalama wa wanafunzi lakini ni miaka miwili sasa hawana bati za
kuezekea majengo hayo waliyoyajenga.
Aidha Bw.Magnas aliiomba Serikali kukitupia jicho kijiji
hicho kwa kukisaidia kutokana na kusahaulika kwa miaka mingi ili wananchi waweze
kujitambua kuwa wao ni watanzania kama walivyo watanzania wengine na
wanastahili kupata huduma za Maji safi na salama,Afya na shule nzuri yenye
walimu kama vijiji vingine.
No comments:
Post a Comment