Monday, October 22, 2012

KAMPUNI YA KICHINAYATISHIWA MBEYA KATIAK UJENZI WA BARABARA

 
 Naibu  waziri  wa ujenzi Eng. Lwenge


SERIKALI imetishia kuinyang’anya kampuni ya China Communication
Construction Limited zabuni ya ujenzi wa barabara ya kutoka Mbeya
mjini hadi Lwanjilo wilaya ya Mbeya Vijijini yenye urefu wa kilometa
36 baada ya kutoridhishwa na kasi ya utendaji kazi ya mkandarasi huyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Injinia Greyson Lwenge valisema hayo wakati
wakati alipotembelea bara bara  hiyo juzi na kusema kuwa  hatua ya
Serikali imetokana na mkandarasi huyo kushindwa kufikia malengo ya
ujenzi huo kwa kiwango cha lami katika muda uliopangwa huku akiwa
tayari ameshakabidhiwa fedha za awali za mradi huo shilingi bilioni
Nane za Tanzania.

Ujenzi huo unaogharimu zaidi ya sh.bilioni 55 zilizotolewa na Serikali
/>ya Tanzania kwa kushirikiana na Wahisani wa maendeleo ni sehemu ya
mradi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mbeya mjini hadi wilayani Chunya
yenye urefu wa kilometa 72.

Sehemu ya pili ya ujenzi huo kutoka Lwanjilo hadi Chunya mjini
utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 44 kupitia mkandarasi mwingine.


Mkandarasi huyo aliyeanza kazi hiyo Novemba mwaka jana amechukua
nafasi ya mkandarasi wa awali kampuni ya Kundan Sing iliyokabidhiwa
ujenzi huo mwaka 2010 kabla ua kushindwa kuendelea na kazi kutokana na
Serikali kuchelewa kutoa fedha mradi huo.


Hata hivyo tangu alipokabidhiwa kazi hiyo, kasi ya utendaji wake
imekuwa ikilalamikiwa na mamlaka husika kwa maelezo kuwa ameshindwa
kuifanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

Akikagua ujenzi huo  Injinia Greyson Lwenge, alisema
Serikali hairidhishwi na kasi ya utendaji kazi ya mkandarasi huyo na
kutishia kumnyang’anya zabuni hiyo.

“Nimetembelea ujenzi huu kwa kilometa zote 36 kutoka Mbeya mjini hadi
hapa Lwanjilo, ukweli sijaridhishwa na kazi inavyokwenda, mvua
zinakaribia kunyesha na hakuna mafanikio yaliyofikiwa kama
tulivyotarajiwa.”

“Serikali imeshatangaza kuwa barabara hii ni lazima ikamilike kwa
wakati, hivyo kama tutaona mkandarasi huyu anaendelea kusuasua,
hatutasita kumnyang’anya kazi na kumtafuta mkandarasi mwingine,
tunataka kazi ifanyike hatutaki maneno.” alisema Injinia Lwenge.

Hadi sasa mkandarasi huyo amenza ujenzi wa barabara hiyo katika kijiji
cha Lwanjilo katika urefu usiozidi kilometa tano hali inayoitia shaka
Serikali kuwa huenda isikamilike kwa wakati katika kipindi cha miezi
36 tangu alipokabidhiwa zabuni hiyo Novemba mwaka jana.

Kutokana na hali hiyo Injinia Lwenge ameiagiza Wakala wa Barabara
nchini, TANROADS mkoa wa Mbeya na Mhandisi wa mkoa kuhakikisha
mkandarasi huyo anatekeleza kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba uliopo
pamoja na kuhakikisha barabara hiyo haifungwi wakati wa mvua ili
kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Hata hivyo viongozi wa kampuni hiyo ya China Communication
Construction Limited hawakuwa tayari kuzungumza na Waandishi wa habari
kuhusu hali hiyo huku wakishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu
kuchelewa kuanza kwa ujenzi huo wakati wakizungumza na Injinia Lwenge.

Awali mmoja kati ya viongozi wa kampuni hiyo ambao pia hawakuwa tayari
kutaja majina yao, alijifanya hajui kuzungumza lugha ya Kiingereza na
kutumia mkalimani kumjibu Injinia Lwenge kabla ya Naibu Waziri huyo
kubaini ujanja huo na kumlazimisha kuzungumza lugha hiyo na hatimaye
kufanya hivyo kwa ufasaha mkubwa.

Barabara hiyo ni miongoni mwa barabara zilizomo kwenye Ilani ya
Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, CCM, ya mwaka 2010 ambapo Rais Jakaya
Kikwete, aliwaahidi wakazi wa vijiji vinavyopitiwa na barabara kuwa
atahakikisha inatengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuwaondoakuwa
atahakikisha inatengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuwaondolea kero
ya usafiri hasa wakati wa mvua.

Ubovu wa barabara hiyo umesababisha wakazi wa kijiji cha Lwanjilo
kutozwa kati ya shilingi 8,000 hadi 10,000 kwenda Mbeya mjini umbali
wa kilometa 36 wakati nauli ya kutoka Mbeya mjini hadi wilayani Kyela
umbali wa zaidi ya kilometa 110 ikiwa ni shilingi 3,000.

No comments:

Post a Comment