CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA NJOMBE LEO KIMECHAGUA VIONGOZI WA MUDA WAKATI MCHAKATO WA UUNDWAJI KATIBA NA USAJILI WA CHAMA HICHO UKIENDELEA
NI UCHAGUZI WA MUDA KAMA HATUA YA MAANDALIZI YA USAJILI WA CHAMA HICHO PAMOJA NA MCHAKATO WA UANDAAJI WA KATIBA YA CHAMA.
Hii ni timu ya baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Njombe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwanahabari mwenzao Deo Haule Filikunjombe ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Ludewa akiwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa uchaguzi huo Leo.
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe aliyesimama katikaakiwa na wanahabari wa mkoa wa Njombe mara baada ya kuunda chama cha waandishi wa Habari mkoa huo Njombe Press Club.
Aliyesimama hapo juu ni katibu wa chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Iringa Bwana Frank Leonard akizungumza na wanahabari wa Mkoa wa Njombe wakati wa uchaguzi wa viongozi.
Aliyesima hapo juu ni Makamu katibu wa chama cha waandishi wa Habari wa mkoa wa Njombe Lilian Mkusa mara baada ya Kuchaguliwa leo.
Msimamizi wa uchaguzi huo huyo hapo juu bwana Fredrick James Siwale ambaye ni mwakilishi wa RFA na STAR TV kutoka Njombe akiwataka wanahabari kuwa makini na kazi zao.
Hapo juu ni Mtunza Hazina aliyechaguliwa na chama cha waandishi wa habari leo bwana Sunday Bavuga wakati akijinadi.
HAPA ni katibu wa NJOMBE PRESS CLUB NPC Hamis Hassan Kassapa mara baada ya kupita bila kupingwa.
Huyo hapo ni Consolatha Kihombo ambaye naye achaguliwa kuwa msaidizi wa mtunza hazina
Hapa ni Mwenyekiti aliyevalia shati na Katibu wa chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe bwana Hamis Kassapa wakiwa kazini mara baada ya kushinda na kuanza rasmi kazi.
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe, Njombe Press Club NPC Leo Kimefanya Uchaguzi wa Viongozi wa Muda wa Chama Hicho Ambapo Bazil Makungu Amechaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa NPCkwa kushinda kwa kura 20 19 kati ya 20 zilizopigwa Huku Ellymathew Kika Akichaguliwa Kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kushinda kura 8 na kuwabwaga wagombea wenzake watatu..
Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi Huo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Huo Shaban Lupimo Amesema Mwenyekiti wa Muda wa NPC Bazil Makungu Amepata Kura 19 Kati ya Kura 20 Zilizopigwa Huku Kura Moja Ikiharibika.
Amesema kwa nafasi ya katibu wa chama hicho Ndg.Hamis Hassan Kassapa ameshinda kwa kura 15 kati ya 18 zilizopigwa na tatu kuharibika kutokana na mgombea kuto kuwa na mpinzani huku Lilian Mkusa akichaguliwa kuwa makamu Katibu.
Katika nafasi ya uhasibu Sunday Bavuga amechaguliwa mara baada ya kukosekana kwa mpinzani huku Consolatha kihombo akichaguliwa kuwa makamu wake.
Kwa Upande Wake Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Huo Fedrick Siwale ametangaza Majina ya Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji wa Njombe Press Club watakao ingia kwenye kamati hiyo.
Wajumbe hao ni wale saba watakaokamilisha safu ya watendaji 13 wa chama hicho ambao ni pamoja na Festus Pangan,Nickson Mahundi,Gabriel Kilamlya,Riziki Manufred,Amos Kaposo,Martha sanga pamoja na Mercy James,
Awali Akizungumza Kabla ya Uchaguzi Huo Mgeni Rasmi Deo Haule Filikunjombe Ambae ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Amewataka Waandishi wa Habari Kufanyakazi Kwa Zingatia Maadili, Mipaka, Misingi ya Taaluma Yao Pamoja na Kutumia Weledi Walionao.
Katika Hatua Nyingi Filikunjombe Ameahidi Kutoa Vifaa Kwa Ajili ya Ofisi ya Waandishi wa Habari Zikiwemo Kompyuta Ndogo (Laptop), Printer na Scannaer pamoja na vifaa vingine.
Akizungumza Kwaniaba ya Viongozi Waliochaguliwa Mwenyekiti wa NPC Bazil Makungu Amewashukuru Wajumbe wa Chama Hicho na Kuwataka Kuwa na Ushirikiano Kati Yao na Viongozi Waliowachagua Ili Kufanikisha Malengo ya Chama Hicho.
Uchaguzi Huo Umehudhuriwa na Wageni Kutoka Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa ICP Akiwemo Katibu wa ICP Frank Leonald
No comments:
Post a Comment