Akuffo akishangilia bao lake |
Akuffo akishangilia huku akifuatwa na Juma Nyosso kupongezwa |
Nassor Masoud 'Chollo' anatia krosi |
Chollo anatia krosi |
Okwi anashangilia bao lake |
Ngassa anafunga akiunganisha krosi ya Chollo |
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Ngassa (16)n kwa kufunga bao la pili. Kushoto kabisa ni mtoaji wa pasi Chollo akimuwahi kumpongeza |
Okwi anapasua |
Kikosi cha Lyon leo |
Kikosi cha Simba leo |
Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA SC
imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni
hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi
hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi
mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na
Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Mrisho Ngassa
dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, ambayo tayari
ilikuwa na mwelekeo wa kutinga nyavuni.
Lyon
walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na
Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha
pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala
mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffo aliifungia timu yake bao la kuhitimisha
ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la
hatari.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna
Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na
Emanuel Okwi.
African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi
Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa,
Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.
Katika mechi
nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul,
Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar
Khalfan, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu na Stefano
Mwasyika.
Kwenye Uwanja
wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa
1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni,
Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao, John
Bocco, Abdi Kassim na Kipre Herman Tchetche.
No comments:
Post a Comment