Baada ya kukamilisha usaili Dodoma, Kahama,
Kagera,Singida, Mwanza, Morogoro, Iringa sasa usaili unaelekea mkoani
Mbeya ambapo utafanyika Sept 15 .
Crew nzima ya Maisha
Plus/Mama Shujaa wa Chakula inayodhaminiwa na banki ya NMB na Oxfam
baada ya hapo itaendelea na safari kutoka Mbeya moja kwa moja mpaka
Kilwa, ambapo itafanya usaili Septemba 17, kesho yake yaani Septemba 18
usaili utaelekea Masasi mkoani Mtwara.
Septemba 20 itakuwa zamu ya
Wanzanzibar kusailiwa katika kumpata mwakilishi wa Maisha Plus kisha
timu itarejea Dar tayari kwa usaili ambao utafanyika Septemba 22 na 23.
Kitakachofuata baada ya usaili wa Dar ni kipindi cha Maisha
Plus/Mama Shujaa wa Chakula kuanza kuonekana kwenye runinga yako.
Usikae mbali na TBC1
kwasababu ndiyo itakayokusafirisha nchi nzima..
Wakati usaili ukiendelea
mikoani nchini, Huko nchini Burundi nako usaili wa kuwapata washiriki
wawili ulikuwa unafanyika kwa maana hiyo safari hii shindano la Maisha
Plus litakuwa na washiriki kutoka huko.Huu ni mwanzo wa shindano hili
wa kuzishirikisha nchi zote za Ukanda wa Mashariki ya Afrika.
Kwa wakazi wa Dar fomu za
ushiriki zinapatikana katika duka la Masoud Kipanya lililopo Millenium
Tower, Kijitionyama.
Unaweza kupata usaidizi ka kupiga namba
hii 0717 710303.
Usikose kupitia hapa kila mara kwa ajili
ya updates za kipindi chako kizuuri kabisa cha Maisha Plus....
No comments:
Post a Comment