HAMU ya klabu kubwa za Uingereza kujiimarisha inaendelea, ambapo Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anaitaka klabu hiyo imsajili Cristiano Ronaldo.
Suala la usajili limeendelea kugonga vichwa vya habari, hata baada ya dirisha kufungwa, na sasa Ferguson anataka klabu ifanye lolote kumrejesha Old Trafford Mreno huyo.
Ronaldo anayekipiga Real Madrid chini ya kocha mwenye majigambo, Jose Mourinho ‘The Only One’, amenukuliwa akisema hana raha klabuni hapo.
Taarifa kumhusu Ronaldo kurejea tena Ligi Kuu ya England (EPL) zilianza na tetesi kwamba Roberto Mancini wa Manchester City alikuwa akiandaa kitita cha kufuru kumvuta nyota huyo.
Ferguson kuingia mchezoni sasa, kunaligeuza suala hili kuwa moja ya tetesi kubwa zaidi kuhusu usajili, ambapo muda unaolengwa kutekeleza mpango huo ni dirisha dogo la Januari mwakani.
Ronaldo alitokea kuwa mwanasoka ghali zaidi duniani, aliyekipiga Manchester United tangu 2003 hadi 2009 alipouzwa Real Madrid kwa £80 milioni.
Ferguson ana sauti kubwa klabuni hapo, lakini kuitaka bodi kumrejesha Ronald yaweza kuwa kitu kisichowezekana.
Ikumbukwe kwamba, ni Ronaldo huyu aliyekwishafunga mabao 150 katika Ligi Kuu ya Hispania – La Liga.
Ni katika hadhi hiyo, mapato yake yanaweza kusemwa kuwa ni matawi ya juu, kwani kwa wiki anakunja kitita cha £500,000, na bei yake inaweza kuwa haishikiki.
Ombi la Ferguson laweza kuwa kuwatonesha kidonda Manchester United, kwani wanachaganyikiwa kwa madeni yanayowakabili.
Hata hivyo, kama kweli Ronaldo anavyosema kwamba ukosefu wake wa raha si kutaka fedha nyingi, anaweza kuwatonya United, nao watawasilisha dau lao Santiago Bernabeu.
Lakini yote hayo yanakuja wakati Ronaldo na klabu yake wakitayarisha kauli ya pamoja, ili kuwatoa wadau wa Real Madrid katika mtanziko waliotiwa na habari za hivi karibuni kuhusu nyota huyo.
Klabu inapenda na inalenga kuongeza mkataba wake kupindukia mwaka 2015, wakati ikimuunga mkono kwa tuzo mbalimbali.
Zipo habari kwamba simanzi ya Ronaldo ni kutokuwa katikati ya nyota wengine, wa aina ya Lionel Messi na Andres Iniesta.
Hata hivyo, kuna suala la sheria mpya za kodi. Hivi sasa Ronaldo anaaminika kupata fedha raslimu £8,000,000 kwa mwaka, baada ya kodi ya kama milioni mbili hivi.
Lakini, ikiwa Ronaldo atapata nyongeza ya mshahara taslimu anaochukua nyumbani kwa asilimia 30 (£10.35 milioni kwa mwaka( utaigharimu Real Madrid zaidi ya £20,000,000) kwa mwaka. Yaweza kuwa biashara kichaa kwa mabingwa hao wa Hispania.
Sasa basi, ikiwa Mashetani Wekundu wanamtaka Ronaldo kweli, maana yake ni kwamba hatma Nani (LuÃs Carlos Almeida da Cunha) klabuni hapo itakuwa imewadia.
Ferguson anaona kwamba Nani haisaidii sana timu, na amekuwa akimwacha benchi kama chaguo la pili au hata la tatu.
Lakini Nani mwenyewe alijaribu kutafuta pa kutokea kabla dirisha kufungwa akakosa, na alidaiwa kuwa tayari kupunguza mshahara ili abaki Old Trafford.
Katika tetesi nyingine za usajili, yaelekea Florent Malouda wa Chelsea akarejea klabu yake ya awali ya Lyon ya Ufaransa, baada ya Chelsea kumpa kisogo.
Alilalamika kwenye mtandao wa jamii kwamba amepangiwa kufanya mazoezi na timu ya vijana, ambapo ameachwa katika orodha ya wachezaji wa Kombe la Ulaya. Hata hivyo, itabidi avumilie hadi Januari.
Swansea inayotamba katika nafasi ya pili kwenye EPL, inaelekea itamnyakua Dwight Tiendalli kuziba pengo la beki wake, Neil Taylor aliyeumia. Tiendalli ameachwa kama mchezaji huri na klabu yake ya FC Twente ya U
No comments:
Post a Comment