Tuesday, June 14, 2016

WanaMakete Kuitetemesha Mbeya.


Mimi na Dada yangu Linah Sanga "Malkia wa Nguvu" tutashirikiana kwenye Uzinduzi wa Mradi Mkubwa kuwahi kutokea katika nyanda za juu kusini Mradi wa DREAMS.
DREAMS ni mradi unaowalenga wanawake vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 wenye nia ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoweza kuwapelekea kupata maambukizi ya UKIMWI.
Uzinduzi utafanyika Siku ya Mtoto wa Afrika June 16 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe ukitanguliwa na maandamano yatakayoanzia Kituo cha daladala cha Kabwe. Linah atafanya shughuri nyingi za kijamii ikiwemo kushiriki semina kadhaa, kufanya mazungumzo na makundi mbali mbali ya vijana walio nje ya mashule. Atafanya mahojiano kadhaa na redio zilizopo hapa Mbeya na Kisha kupanda Jukwaani siku ya June 16.
Kwa wanamakete wanaotaka kuonana na Dada Linah waliopo hapa Mbeya tunaweza kutafuta muda jioni tukapiga naye story
taarifa hizi ni kwa mujibu wa 
 
    pia mtandao wako wa www.rizikimgaya.blogspot.com utakuletea moja kwa moja yote yatakayojiri katika uzinduzi huo
Jackson Taifa Mbogela

No comments:

Post a Comment