Tuesday, July 7, 2015

JOSE MOURINHO AONGEZA MIAKA 4 CHELSEA


Jose Mourinho akiwa na Kombe la Ligi Kuu ya England msimu uliopita.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesaini mkataba wa miaka minne kuendelea kuifundisha timu hiyo ya London.
Mkataba huo wa Mourinho utamfanya aweke kibindoni kiasi cha Pauni milioni 8.5 kwa mwaka.

Taarifa zimeeleza kuwa Mourinho ameongezewa mkataba huo baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu ya England msimu uliopita.
Katika msimu huo uliopita, Mourinho alitwaa pia Kombe la Ligi.

Kocha huyo ataingia mzigoni akiwakaribisha vijana wake kwa maandalizi ya msimu ujao Jumanne ijayo kabla ya timu yake kuanza ziara yake nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment