MDHIBITI na Mkaguz
i Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa
Mussa Assad, ameamua kuiorodheshea Serikali mapendekezo yote ya
mtangulizi wake, Ludovic Utouh, ambayo hayajatekelezwa na Serikali tangu
2008 na kusisitiza sasa yatekelezwe.
Katika mapendekezo ya mwaka 2009/2010, Profesa Assad, amelalamikia
kitendo cha Serikali kuendelea kuruhusu mwanya wa mgongano wa maslahi,
kwa kuendelea kuteua wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika na
taasisi za umma.
“Bunge ndio chombo cha juu kinachowakilisha wananchi na chenye
majukumu ya kutathimini utendaji kazi wa Serikali, ikiwa ni pamoja na
mashirika na taasisi nyinginezo za umma kupitia kamati za kudumu za
Bunge.
“Ili kuepuka mgongano wa kimaslahi, nasisitiza mapendekezo yangu
kuwa, wabunge hawastahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi
katika mashirika na taasisi nyinginezo za umma, kwani wana jukumu la
kusimamia mashirika hayo,” amesema Profesa Assad.
Posho sawa Akielezea mapendekezo ya mwaka 2008/2009 ambayo
hayajafanyiwa kazi, Profesa Assad ameitaka Serikali kuhakikisha kuwa
kuna uwiano katika marupurupu wanayopata menejimenti na bodi za
wakurugenzi za taasisi za umma.
“Hii inatokana na ukweli kuwa rasilimali wanazotumia kama posho za
vikao, ada za bodi za wakurugenzi na nyinginezo, ni rasilimali za umma,”
alisema Profesa Assad.
Alisema hatua ya Serikali kuanzisha Bodi ya Uwiano wa Mishahara na
Marupurupu, itasaidia kuondoa tofauti zilizopo sasa za kuongeza ufanisi
na uwajibikaji katika mashirika na taasisi nyinginezo za umma.
Wanaodaiwa Bodi ya Mikopo Kuhusu kutorejeshwa kwa mikopo ya Sh
bilioni 51, iliyokopwa na wanafunzi wa zamani wa vyuo vikuu, ambao sasa
hivi ni waajiriwa au wamejiajiri, Profesa Assad aliishauri Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuwachukulia hatua za kisheria
waajiri na wakopaji binafsi, ambao hawatoi ushirikiano.
Alitaka hatua hiyo ichukuliwe kwa kuzingatia Sheria Namba 9 ya Bodi
hiyo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Kuhusu mkopo uliokopeshwa
katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wa Sh bilioni 54
kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Wanafunzi wa Umma (PSPF), alitaka Serikali
irejeshe mkopo wote na riba.
Adhabu TPA Kuhusu mapendekezo ya mwaka 2010/2011, Profesa Assad
alirejea ukaguzi wa mwaka huo, uliobaini kuwa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) ilifanya ununuzi wa dharura milioni 13 bila idhini kutoka
kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali. “Sina taarifa ya hatua zilizochukuliwa
kuhusu suala hilo la ununuzi wa dharura wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,”
amesema.
Katika mwaka huo huo, Profesa Assad alihoji kwa nini Waziri wa zamani
wa Kilimo, Hifadhi ya Chakula na Ushirika, ameendelea kukaa katika
nyumba ya Bodi ya Sukari Tanzania, iliyopo Kiwanja 482 Barabara ya Bray
Masaki.
Mgogoro wa UDA Profesa Assad pia aliendelea kuhoji uuzwaji wa hisa za
Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), uliofanywa na Bodi ya
Wakurugenzi wa shirika hilo bila kupata kibali cha Serikali. Alisema
hisa za UDA zilikuwa na thamani ya Sh 744.79 kila hisa Oktoba 2009 na
ilipofika Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikawa Sh 656.15.
Kwa mujibu wa Profesa Assad, katika uuzwaji wa hisa hizo, Bodi ya
Wakurugenzi iliamua kutoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa, bila
kuwepo kwa sababu ya kufanya hivyo.
Profesa Assad alieleza kuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali alipoulizwa,
alisisitiza kuwa hatambui uuzwaji wa hisa hizo na Serikali inaandaa
mapendekezo ya kuuza asilimia 49 ya hisa za UDA, na itafikisha
mapendekezo hayo katika Baraza la Mawaziri.
“Majibu haya (ya Mlipaji Mkuu wa Serikali), hayasemi chochote kuhusu
mustakabali wa hisa ambazo zilishauzwa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya
wakurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa UDA,” alisema.
Benki ya Azania Profesa Assad pia alihoji inakuwaje mashirika ya
pensheni yameanzisha Benki ya Azania, halafu benki hiyo ikaanzishwa kama
kampuni binafsi na kuachwa kuwa katika orodha ya mashirika
yanayosimamiwa na Msajili wa Hazina.
Kwa mujibu wa Profesa Assad, benki hiyo ambayo awali iliitwa 1st
Adili Bancorp Limited, wanahisa wake ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
hisa asilimia 34.8, Mfuko wa Pensheni wa PPF hisa asilimia 30.1, Mfuko
wa Pensheni wa PSPF hisa asilimia 17.2, Mfuko wa Pensheni wa LAPF hisa
14.2, Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) hisa 2.3 na
wafanyakazi wa Benki ya Azania na wanahisa wengine wenye asilimia 1.4.
CAG katika hilo aliweka wazi kuwa mifuko ya pensheni, ndiyo yenye
hisa nyingi sawa na asilimia 96.3, na hivyo ndiyo yenye nguvu ya kutoa
miongozo na kusimamia benki hiyo na kwa kuwa mifuko yote ya pensheni
inamilikiwa na Serikali, ni wazi benki hiyo ni mali ya Serikali.
Kutokana na mazingira hayo, Profesa Assad alihoji kwa nini benki hiyo
haijawahi kuwasilisha hesabu Zake katika ofisi ya CAG tangu 1995
ilipoanzishwa, kwa ajili ya ukaguzi kama Katiba inavyotaka

No comments:
Post a Comment