HOJA ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika
(CHADEMA) kuhusiana na suala la tatizo la upatikanaji wa maji katika Mkoa wa
Dar es Salaam, inaelekea kupata ufumbuzi kutokana na Rais Jakaya Kikwete
kumuita Ikulu mbunge huyo Jumatatu wiki ijayo.
Wengine
walioitwa kukutana na rais ni Mkuu wa Mkoa, Mecky Sadick, wakuu wote wa wilaya
pamoja na wabunge na wataalamu kutoka Wizara ya Maji.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa daraja la Mtaa wa Golani, Kata ya
Saranga, Rais Kikwete alisema kuwa kutokana na wananchi wa kata hiyo kupiga
kelele kuhusiana na suala la maji ameamua kukutana na viongozi hao ili kupatiwa
ufumbuzi.
Kikwete
pia alitaka kuwepo na mfumo maalumu wa mabomba ya maji yatakayojengwa kwa
saruji kutoka Ruvu Chini na kuja jijini Dar es Salaam moja kwa moja bila
kuchepuliwa sehemu yeyote.
Katika
hatua nyingine, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa wizi wa maji katika maeneo
ambayo mabomba ya maji yamepita.
“Watu
wasifanye ukanjanja katika masuala ya maji, mabomba yanatandazwa na watu
wanaiba maji, shida inayotokea ni maji hayo kutokufika jijini Dar es Salaam,”
alisema.
Alifafanua
kuwa lita milioni 65 zinahitajika ili kukabiliana na tatizo la maji na kwamba
upanuzi wa Ruvu Juu na Chini ujenzi wake utakamilika Julai na kutaka hatua za
haraka kuchukuliwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa haraka ili kumaliza
tatizo.
Hatua
ya Mnyika kuitwa Ikulu imetokana na kusimama kidete katika suala la maji ambapo
Aprili 4, mwaka huu aliwasilisha hoja binafsi na kuitaka serikali kuchukua
hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji
taka katika Jiji la Dar es Salaam hoja ambayo ili iliondolewa bungeni kibabe.
No comments:
Post a Comment